Kumbukumbu ya miaka 65 tangu DRC ipate uhuru wake inafanyika wakati ambapo baadhi ya maeneo ya majimbo ya Kivu kaskazini na Kivu kusini mashariki mwa nchi hiyo yakiwa chini ya waasi wa AFC/M23 huku juhudi za kutafuta amani zikiwa zimeendelea huko Marekani na Doha, Nchini Qatar.