MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
DRC na M23 watia saini mpango wa kusitisha mapigano
19 Julai 2025Matangazo
Tamko hilo la pamoja limesainiwa leo Jumamosi mjini Doha, licha ya taarifa za awali kueleza kuwa bado kulikuwa na masuala kadhaa muhimu ambayo bado yalihitaji kujadiliwa. Hatua hiyo ni ishara ya maendeleo baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo ya amani Kongo chini ya upatanishi wa Qatar.
Na imefikiwa huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani ili kukamilisha makubaliano ambayo yatawezesha kuleta amani mashariki mwa Kongo na hivyo kufanikisha miradi ya uwekezaji wa mabilioni ya dola kutoka kwa mataifa ya Magharibi katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.