MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
DRC: Waasi wa M23 wawarejesha Rwanda wapiganaji 20 wa FDLR
1 Machi 2025Matangazo
Kulingana na Oscar Mugaba Balinda, msemaji wa M23, miongoni mwa maafisa waliokabidhiwa kwa mamlaka za Rwanda ni Jenerali Ézéchiel Gakwerere, kamanda mkuu wa FDLR, ambaye alikamatwa.
Hii si mara ya kwanza kwa wapiganaji wa FDLR kukamatwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC). Kwa mujibu wa Oscar Balinda, wengine walikamatwa huko Bunagana na kurejeshwa Rwanda chini ya usimamizi wa CICR.
Kwa miaka mingi, Rwanda imekuwa ikilalamika kuwa kundi hilo la FDLR, ambalo inaaminika linaundwa na makundi yaliyotekeleza mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, limekuwa likiendesha operesheni zake mashariki mwa Kongo na kutishia usalama wa Rwanda.