Kiongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Moise Katumbi, amehukumiwa kutokana na mzozo wa rasilimali, ardhi na majengo. Mahakama inadai alimuuzia mtu nyumba ambayo si yake.
Kutoka Lubumbashi Sudi Mnette amezungumza na kiongozi wa muungano wa vyama 15 vinavyomuunga mkono Katumbi vijulikanavyo kama G7, Kyungu Wa Kumwanza, na kwanza alitaka kujua wameipokeaje hukumu hiyo.