DR Kongo na M23 zatoa ahadi ya pamoja ya kusitisha mapigano
24 Aprili 2025Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi wa M23 zimetoa taarifa ya pamoja zikisema zimekubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa nchi hiyo wakati zikiendelea na juhudi za usitishaji wa kudumu wa mapigano.
Tangazo hilo linafuatia mazungumzo ya upatanishi yaliyosimamiwa na Qatar ambapo pande zote mbili zilisema "zimekubaliana kufanyia kazi juhudi za kufikia makubaliano" katika mzozo huo ambao umepelekea waasi wa M23 wanaotajwa kuungwa mkono na Rwanda kuteka miji muhimu mashariki mwa nchi hiyo.
Soma pia: Tetesi za Kabila kuwasili Goma zazusha mivutano Kongo
Taarifa hii ya hivi punde imesema pande zote mbili zimethibitisha kujitolea kwao kusitisha mapigano mara moja na kusitishwa kwa uhasama baina yao katika muda wote wa mazungumzo.
Mwanzoni mwa mwezi huu Qatar ilichukua jukumu la kidiplomasia na kusimamia juhudi za upatanishi baina ya pande hizo mbili.