Makubaliano yaliyotiwa saini huko Doha yamekuwa yakitafsiriwa tofauti na pande mbili. Serikali ya Kinshasa wanadai kuwa matakwa yao yalizingatiwa ikiwa ni pamoja na kuvitaka vikosi vya Rwanda na M23 kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia mashariki mwa Kongo, madai yaliyokanushwa vikali na wasemaji wa AFC/M23. Je, makubaliano hayo yatafulu kweli kuleta amani?