DORTMUND. Mwanamume wa Iran afikishwa mahakamani Ujerumani.
13 Aprili 2005Matangazo
Mwanamume mmoja raia wa Iran amefikishwa mahakamani hii leo katika mji wa Ennepetal kwa kuwateka nyara wasichana wanne wa shule wa umri kati ya miaka 11 na 16. Waongoza mashtaka wamependekeza jamaa huyo ahamishwe katika kliniki ya matibabu ya wagonjwa walio na matatizo ya akili. Mwanamume huyo wa miaka 50 aliwateka nyara wasichana hao akitaka jamii yake ijunge naye hapa Ujerumani. Mateka wote wanne waliokolewa wakiwa salama salimini na kikosi maalumu cha usalama, kilichoivamia nyumba alimokuwa mwanamume huyo.