DORTMUND: Angela Merkel aahidi kuuboresha uchumi wa Ujerumani
29 Agosti 2005Matangazo
Angela Merkel, mwanamke wa kwanza kugombea ukansela hapa Ujerumani ameapa kuuboresha uchumi wa taifa. Amesema atafanya kila awezalo kuitoa Ujerumani kutoka kile alichokielezea kuwa hali mbaya zaidi ya uchumi tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.
Merkel alisema katika mkutano wa chama mjini Dortmund kwamba serikali ya muungano wa vyama vya SPD na Kijani chini ya uongozi wake kansela Gerhard Schöder, imeshindwa kutimiza ahadi yake ya kupunguza ukosefu wa ajira.
Matokeo ya kura ya maoni iliyofanywa hivi karibuni, yanaonyesha kwamba muungano wa vyama vya CDU na CSU una nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi utakaofanyika tarehe 18 mwezi ujao.