MigogoroKimataifa
Donald Trump na Putin wazungumza kwa njia ya simu
19 Mei 2025Matangazo
Rais wa Marekani Donald Trump amefanya mazungumzo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin muda mfupi uliopita juu ya kumaliza vita nchini Ukraine.
Mapema leo, Trump aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba anatumai mazungumzo yake na Putin yatafaulu kufikiwa kwa makubaliano ya pande mbili ya kusitisha kwa vita.
Hapa barani Ulaya, viongozi wa Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Italia walizungumza mapema na Trump kabla ya mazungumzo yake na Putin, na wanatarajiwa kuzungumza tena hapo baadaye kupata mrejesho.
Katika hatua nyingine, Trump pia atazungumza pia na viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO na rais wa Ukraine Volodymir Zelenskyy hapo baadaye.