Dominiki yayatangaza makundi yenye silaha Haiti kuwa magaidi
28 Februari 2025Tangazo hilo lililotolewa siku ya Alkhamis (Februari 28) na Rais Luis Abinader linamaanisha kuwa wanachama wa makundi hayo watakaovuuka mpaka na kuingia Dominiki wanaweza kushitakiwa kwa kutumia sheria za kigaidi za nchi hiyo ambazo zinatowa adhabu ya vifungo vya muda mrefu jela.
Rais Abinader anafahamika kwa kupigania kuwepo kwa msimamo mkali wa kimataifa dhidi ya Haiti tangu alipoingia madarakani mwaka 2020, zikiwemo hatua za kuwafukuza maelfu ya raia wa Haiti na ujenzi wa ukuta wa kangiriti kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.
Soma zaidi: Kikosi kipya cha maafisa wa polisi 144 kutoka Kenya chafika Haiti
Udhibiti wa makundi yenye silaha umeongezeka, ukiwemo kwenye mji mkuu Port-au-Prince, licha ya kuwasili kwa mamia ya polisi wa kimataifa wanaoongozwa na vikosi vya Kenya.
Mwaka jana pekee, Umoja wa Mataifa uliripoti vifo vya watu 5,600 vinavyohusishwa na makundi hayo.