DNJAMENA:Makumpuni mawili ya mafuta yafukuzwa Chad
27 Agosti 2006Matangazo
Serikali ya Chad imeziamrisha kampuni mbili za mafuta kuondoka nchini kufuatia mzozo juu ya kodi.
Rais Idriss Deby ameziambia kampuni za Chevron Texaco ya Marekani na Petronas ya Malaysia zifunge virago na ziondoke Chad kwa sababu ya kukataa kulipa kodi.
Kampuni hizo zinashughulikia asilimia 60 ya uzalishaji wote wa mafuta nchini Chad.
Serikali ya Chad imekuwa na mikwaruzano ya mara kwa mara na kampuni za mafuta kutoka nje juu ya mapato yanayotokana na mauzo.