Dembele aondoa hofu ya jeraha dhidi ya Arsenal
30 Aprili 2025Dembele alifunga bao la mapema katika ushindi wa 1-0 dhidi ya washika bunduki uwanjani Emirates, matokeo ambayo yanaifanya PSG kuwa katika nafasi nzuri kuelekea mechi ya marudiano Jumatano wiki ijayo katika uwanja wa Parc des Princess.
Hata hivyo alitolewa kunako dakika ya 70 ya mchezo huku ripoti zikieleza kwamba alipata jeraha la msuli wa nyuma ya paja.
Soma pia: Barcelona na PSG ndani ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa
Dembele hata hivyo ameviambia vyombo vya habari vya Ufaransa kwamba licha ya kuhisi maumivu kidogo, yuko sawa.
PSG inawinda mataji matatu msimu huu; tayari imechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1, na wametinga fainali ya Kombe la Coupe de France dhidi ya Reims itakayochezwa mnamo Mei 24 na pia kuna uwezekano wa kucheza fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Mei 31 mjini Munich.