Dawa ya kwanza ya Malaria kwa watoto wachanga imepata idhini kutoka mamlaka ya afya nchini Uswisi na Kenya ni miongoni mwa nchi za mwanzo za Afrika tayari kutumia dawa hiyo. Mwandishi wetu Wakio Mbogho amezungumza na daktari Willis Akwale ambaye ni mshauri mkuu wa Baraza la End Malaria nchini Kenya kuhusu mchango wa dawa hiyo katika mapambano dhidi ya Malaria.