DARMSTADT/UJERUMANI: Mpaka sasa wakuu wa shirika la Ulaya la utafiti ...
26 Desemba 2003Matangazo
wa anga za juu hawajafanikiwa kupokea ishara kuthibitisha kama chombo chao kimewasili kwenye sayari MARS. Wanasayansi katika kituo cha usimamizi hapa Ujerumani wanangojea mafungamano mengine baadaye hivi leo. Chombo BEAGLE 2 kilitarajiwa kuwasili Mars mapema jana asubuhi. Ujumbe wake ni kuchunguza kama kuna maisha katika sayari hiyo nyekundu.