Damu inazidi kumwagika nchini Afghanistan
18 Agosti 2007Matangazo
Kaboul
Shambulio la mtu aliyejiripua limegharimu maisha ya watu wengine 15 kusini mwa Afghanistan.Duru za polisi zinasema watu wengine 25 wamejeruhiwa.Wengi kati ya wahanga wa shambulio hilo ni raia wa kawaida,wakiwemo waafghani wanaolitumikia shirika la usalama la Marekani.Walikua wawalinde wanajeshi wa kimarekani waliokua njiani kuelekea eneo la machafuko la Helmand.