damu inaendelea kumwagika Iraq
3 Septemba 2005Jumla ya wanajeshi na polisi 20 wa Irak wameuliwa hii leo kufuatia mashambulio matatu mbali mbali huko Baqouba kaskazini mwa Baghdad.Waasi kadhaa pia wameuliwa.Mashambulio hayo yamejiri katika wakati ambapo matumaini ya mshikamano yamezuka baada ya msiba wa jumatano iliyopita ambapo zaidi ya watu 900 waliuwawa.Vikosi zaidi vya jeshi vimepelekwa katika eneo hilo linalodhibitiwa na waasi.Wakati huo huo katika jimbo la kaskazini la Kirkouk,kisima cha kusafishia mafuta cha Baiji kimetiwa moto hii leo.Kwa mujibu wa kepteni Ali Obeidi,vikosi vya zima moto vinaendelea hadi sasa kuzima moto huo ulioanzia Dirbhane,umbali wa kilomita 70 magharibi ya Kirkouk.Mjini Baghdad kwenyewe dhamana mmoja wa shirika la usalama ametekwa nyara.Kuna ripoti pia za kuuliwa watalii wawili wa Japan hii leo.