CUBA:Marekani kuikabidhi Yemen raia wake 7 walioko Guantanamo bay
31 Julai 2005Matangazo
Marekani imekubali kuikabidhi Yemen raia wake saba waliozuiliwa kwenye jela ya Marekani huko GuantanamoBay Cuba.
Waziri wa mambo ya nje wa Yemen Abubakar Al Qirbi amesema maafisa wa serikali wamepokea taarifa rasmi juu ya kukabidhiwa raia hao. Hata hivyo hivyo imesema tarehe haijatolewa.
Takriban wayemen 107 wanasemekana kuwa miongoni mwa wazuiliwa 510 waliopo katika jela ya Marekani ya Guantanamo Bay Cuba.