CRAWFORD-TEXAS: Marekani yaweza kutumia nguvu dhidi ya Iran
14 Agosti 2005Matangazo
Rais George W.Bush wa Marekani amesema matumizi ya nguvu dhidi ya Iran ni hatua anayoweza kufikiria pindi juhudi za kidiplomasia hazitoifanya Iran isitishe mradi wake wa kinuklia.Bush ametamka hayo siku chache tu baada ya Iran kutangaza kuwa imeanzisha tena kazi za kurutubisha madini ya uranium kwenye kinu chake cha Isfahan.Shirika la Nishati ya Kinuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA kwa mara nyingine tena limetoa mwito kwa Iran isimamishe kazi hizo.Iran lakini inasema kuwa ina haki ya kutumia teknolojia ya kinuklia kwa matumizi ya amani.Marekani inaituhumu Tehran kuwa inadhamiria kutengeneza silaha za kinuklia.
.