MigogoroColombia
Colombia kutorefusha mpango wa amani na waasi wa FARC
18 Aprili 2025Matangazo
Hatua hiyo inalihusu kundi lililogawanyika la Wanajeshi wa Mapinduzi ya Colombia FARC na kundi la wapiganaji la EMBF. Makubaliano hayo yamekuwepo kwa mwaka mmoja na nusu na yalichangia pakubwa kurejesha hali ya utulivu nchini humo.
Rais wa Colombia Gustavo Petro amekuwa akijaribu kumaliza mzozo na makundi yenye silaha tangu alipoingia madarakani mwaka 2022, lakini hatua hii ya kusitishwa kwa makubaliano hayo hasa na waasi wa FARC kutafifiza azma hiyo na kuhatarisha usalama. Hata hivyo mamlaka za Colombia zimesema mazungumzo ya amani na makundi hayo yenye silaha yataendelea.