COLOGNE:Baba mtakatifu Benedikt wa 16 Ujerumani
19 Agosti 2005Vijana wapatao laki nne wapo mjini Kologne kuendelea na kongamano la vijana duniani hasa wakikatoliki.
Hotuba ya baba mtakatifu Benedickt wa 16 hapo jana iliwatia moyo vijana kuliendeleza neno la Yesu Kristo.
Baba mtakatifu Benedikt wa 16 ambaye anawaongoza vijana katika kongamano hilo la siku nne amewahutubia viongozi wa madhehebu ya wayahudi mjini Kolon na kuwataka wawe na mshikamano wa dini.
Anatarajiwa pia kukutana na rais wa shirikisho la Ujerumani Horst Kohler na baadae kukutana na wawakilishi 30 wa dini na madhehebu tofauti mjini Kologne.
Kilele cha Kongamano la vijana duniani kitafikiwa jumapili ijayo katika uwanja wa Marien Feld ambapo kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni ataongoza misa maalum mbele ya waumini vijana zaidi ya laki nane kutoka kila pembe ya dunia.