JamiiMarekani
Chuo cha Harvard chaishitaki serikali ya Trump
23 Mei 2025Matangazo
Kesi hiyo inaishutumu serikali kwa kujaribu kukiweka chuo hicho chini ya shinikizo na "ukiukaji wa wazi" wa Katiba ya Marekani.
Mapema Ijumaa, China iliishutumu Marekani kwa kuingiza siasa kwenye sekta ya elimu. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Mao Ning, amesema, hatua hiyo ya utawala wa Donald Trump bila shaka itadhuru sura na hadhi ya kimataifa ya Marekani.
Takwimu za chuo cha Havard ambacho ni miongoni mwa vyuo vikuu bora duniani, zimeonyesha kuwa wanafunzi Elfu sita na mia saba, (6,700) sawa na aslimia 27 ya jumla ya wanafunzi wake wanatoka nje.