Chombo cha anga cha NASA, Voyager 2 charejesha mawasiliano.
5 Agosti 2023Chombo cha anga, Voyager 2 cha shirika la anga la NASA kimerejesha mawasiliano kamili miezi 2 mapema kuliko ilivyotarajiwa, shirika hilo limesema. Mnamo mwezi wa Julai maelekezo ambayo hayakuwa sahihi yalielekezwa kwenye chombo hicho kilichotumwa kuchunguza anga mnamo mwaka wa 1977. Chombo hicho kilibadilisha mkondo na kukata kabisa mawasiliano. Hata hivyo Ishara ilipokelewa Jumanne iliyopita kutokana na mlio wa transmita na kuwezesha antena ya chombo cha Voyager 2, kugeukia duniani. Baada ya mawasiliano kupotea haikuwezekana kwa Voyager 2 kuleta data kwenye mtandao wa shirika la NASA lakini hapo jana shirika hilo lilithibitisha kupokea data kutoka kwenye chombo hicho na kwamba kinafanya kazi kama kawaida. Chombo cha Voyager 2 kilirushwa angani mnamo mwaka 1977 ili kufanya uchunguzi wa sayari nyingine.