SiasaChina
China yatishia kuwashughulikia wanaotaka uhuru wa Taiwan
9 Machi 2025Matangazo
Jeshi hilo limetoa tahadhari hiyo na kuwaonya wanaounga mkono uhuru wa Taiwan kuachana na harakati hizo ili wasiwe hatarini.
Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya taifa ya China CCTV, msemaji wa jeshi Wu Quian amesema kadri watu wanaotaka kujitenga wanavyozidi kuichochea hoja hiyo ndivyo vitanzi kwenye shingo zao vitakavyozidi kuwabana.
Soma pia: Taiwan yasema ndege 45 za China ziliingia anga yake
China imekuwa ikiongeza shinikizo kwa mamlaka za Taiwan na kufanya luteka za kijeshi pamoja na kupeleka ndege na meli za kivita kukizunguka kisiwa hicho.
Beijing inakichukulia kisiwa cha Taiwan kinachojitawala kama sehemu ya himaya yake na imedhamiria kukirejesha hata kwa kutumia nguvu ya kijeshi.