China yatishia kuchukuwa hatua dhidi ya vikwazo vya EU
21 Julai 2025Wizara ya biashara, imesema licha ya pingamizi za mara kwa mara, Umoja huo wa Ulaya imezijumuisha kampuni za nchi hiyo kwenye orodha ya 18 ya vikwazo dhidi ya Urusi pamoja na kuziwekea vikwazo kampuni mbili za China kwa misingi ya shtuma za uongo .
Wizara hiyo imeongeza kuwa China haijaridhishwa na hatua hiyo na itachukuwa hatua za kulinda haki za kampuni zake na taasisi za kifedha.
Mkwamo waongezeka ;Urusi yaonya vikwazo vitawarudia walioviweka
Taarifa hiyo inakuja kabla ya mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na China siku ya Alhamisi mjini Beijing, ambapo Rais wa Baraza laUlaya António Costa pamoja na mwenzake wa Halmashauri kuu ya Umoja huo wa Ulaya Ursula von der Leyen, wanatarajiwa kukutana na Rais wa China Xi Jinping na waziri mkuu Li Qiang.