SiasaChina
China yasema, Kim Jong Un kuhudhuria gwaride la kijeshi
28 Agosti 2025Matangazo
China imesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, atahudhuria na kukagua gwaride kubwa la kijeshi mjini Beijing Septemba 3, wakati wa kumbukumbu ya miaka 80, tangu kumalizika kwa Vita Vikuu Vya Pili vya Dunia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Hong Lei, amesema hayo leo asubuhi kwenye kikao chake na waandishi Habari huko Beijing.
Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kuzuru China tangu mwaka 2019.
Viongozi wengine 26, akiwemo rais wa Urusi Vladimir Putin, pia watahudhuria gwaride hilo, litakaloonesha zana za kisasa za China