Licha ya maandamano makubwa ambayo yameshuhudiwa Hong Kong, China imesema itamuunga mkono kiongozi huyo pamoja na juhudi za serikali yake. Hong Kong imeshuhudia maandamano makubwa ya kumtaka kiongozi wake kujiuzulu, kufuatia muswada wenye utata unaotaka wahalifu wa Hong Kong wastakiwe China bara.