China yalaumiwa kuishambulia ndege ya kijeshi ya Ujerumani
8 Julai 2025Matangazo
Imeishutumu China kuwa ilitumia teknolojia ya mionzi mikali dhidi ya ndege hiyo na kutibua operesheni nzima na kuhatarisha maisha ya Wajerumani waliokuwemo kwenye ndege iliyolengwa. Msemaji wa jeshi la Ulinzi la Ujerumani amesema chombo hicho kilishambuliwa bila sababu katika shuguli zake za kawaida pasipo taarifa. Takriban wanajeshi 700 wa Ujerumani hushiriki kwenye operesheni maalumu ya Umoja wa Ulaya iitwayo Aspides katika Bahari ya Shamu kwa madhumuni ya kuzilinda meli dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Houthi wa Yemen.