SiasaChina
China yajibu vikwazo vya ushuru vya Trump
4 Aprili 2025Matangazo
Katika mzozo kati ya mataifa hayo makubwa kiuchumi duniani, Beijing ilitangaza udhibiti wa usafirishaji wa bidhaa adimu na kuwasilisha malalamiko katika Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Soma pia: Trump atangaza ushuru mpya wa magari yanayoagizwa kutoka nje
China imeongeza kampuni 11 kwenye orodha ya adhabu dhidi ya mashirika ya kigeni, ikiwa ni pamoja na kampuni zinazohusishwa na uuzaji wa silaha kwa Taiwan, ambayo China inadai kuwa sehemu ya mamlaka yake.
Soma pia: China yafanya luteka za kijeshi kuzunguka Taiwan
Canada na China zimekuwa zikijiandaa kujibu hatua ya Marekani kuongeza kiwango cha ushuru.