BiasharaChina
China yaitaka Marekani "kufuta kabisa" ushuru wake wa kisasi
13 Aprili 2025Matangazo
Wizara ya Biashara ya China imesema katika taarifa yake kwamba, inaitaka Marekani ichukue hatua thabiti ya kurekebisha makosa yake na kujirudi katika njia sahihi ya 'kuheshimiana.'
Aidha China iliongeza kwamba msamaha uliotangazwa ni 'hatua ndogo' zilizochukuliwa na Washington na kwamba Beijing, inafanya kile ilichokiita "tathmini za athari" za uamuzi huo.
Soma pia: China yaomba mshikamano na EU kuukabili ushuru wa Trump
Siku ya Ijumaa, Ofisi ya Forodha na Ulinzi wa Mipakani Marekani ilitangaza kuwa vifaa vya kielekroniki ikiwemo simu za mkononi, kipatakilishi yaani laptop, chipu zipo nje ya ushuru wa kimataifa ambao ulianzishwa na Rais Donald Trump mapema mwezi huu.