SiasaAsia
China yagundua eneo jipya la uchimbaji mafuta
31 Machi 2025Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la nchi hiyo, Xinhua, eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita 170, liitwalo Huizhou, lina akiba ya zaidi ya tani milioni 100 za mafuta.
Majaribio ya uchimbaji mafuta yameonesha kuwa matangi 413 ya mafuta ghafi na mita za ujazo 68,000 za gesi asilia hupatikana kwa siku kwenye eneo hilo.
Sehemu yalikogunduliwa mafuta hayo haimo kwenye eneo linalozozaniwa kati yake na Ufilipino, Malaysia, Vietnam na Brunei.