SiasaAsia
China yafanya mazoezi mengine ya kijeshi Taiwan
2 Aprili 2025Matangazo
Msemaji wa Kamandi ya Mashariki ya Jeshi la China, Shi Yi, amesema mazoezi hayo ya leo yana dhamira ya kujaribu uwezo wa jeshi "kwenye uwekaji vizuizi na kudhibiti, na mashambulizi mahsusi dhidi ya maeneo mahsusi."
Sehemu yalikofanyika mazoezi hayo ya leo ni ujia muhimu wa bahari, kwa meli za kibiashara ulimwenguni. Taiwan imesema ndani ya masaa 24 yaliyopita, China imetuma ndege 76 na meli 15 za kijeshi kwenye kisiwa hicho.