China yaahidi kuendelea kuisaidia Urusi
15 Julai 2025Xi amesema China na Urusi zinatakiwa kufanya kazi pamoja kuziunganisha nchi za kusini mwa dunia na kukuza maendeleo ya utaratibu wa kimataifa kwa kuangazia mwelekeo wa haki zaidi na unaofaa.
Viongozi hao wawili wamekutana, wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje wanahudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, SCO mjini Beijing.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema awali kuwa masuala kadhaa yalijadiliwa katika mkutano wa pande hizo mbili, ikiwemo maandalizi ya ziara ya Rais Vladimir Putin nchini China kuhudhuria mkkutano wa SCO, pamoja na maadhimisho ya kumbukumbu ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Wakati huo huo, Iran imesema itafanya mazungumzo na washirika wake wa Asia, Urusi na China, pembezoni mwa mkutano huo, huku Tehran ikitafuta kuungwa mkono kufuatia vita vya siku 12 na Israel mwezi uliopita.